• Elius' Letters
  • Posts
  • Kwa Nini 1% ya Graduates Wanafanikiwa Kuliko 97% ya Wanaobeti?

Kwa Nini 1% ya Graduates Wanafanikiwa Kuliko 97% ya Wanaobeti?

Social Media Marketing businesses za College graduates Tanzania na Dopamination of Tanzanian Young man kwenye Sports Betting

The Dopamination of a Tanzanian Young Man

Kwamfano, Umemaliza chuo, huna ajira, Huna biashara ya kufanya. Huna GPA nzuri ya kuajiriwa na kampuni ya ndoto yako

Alafu ukasikia kuna Million 800 jackpot inatolewa kwa Mshindi kama ukibeti Buku tu. Sema ukweli, si utajaribu bahati yako?

Obviously, utajaribu. Maana ukiwaza hyo 800M ukiipata, jinsi utakavyobadili maisha yako. Hatari

Kwahyo unachukua buku, unaweka beti. Mechi zinaisha ndani ya week ili ujue kama mkeka umetick au umechana

Kwahyo, week nzima unakuwa unatembea ukiwaza 800M, siyo ile buku ulobeti. Na kwakuwa 800M ni game Changer, unatembea ukiwa na dopamine, na Furaha na excitement week nzima

Mpaka huwezi kufanya kitu kingine maana wewe ni Shah Rukh Khan hapa Mjini, Don to be.

Mkeka ukichanika, utaumia dakika nane tu, ubongo wako utasema “Najua tumepata loss, Lakini kumbuka tumeishi kwa Furaha Week Nzima, think positive bro, Tufanye tena hii week”

Inakuwa circle ambayo ni vigumu kutoka

Lakini cha ajabu, hakuna mtu huwa anashinda jackpot kwenye Sports Betting Tanzania.

Honestly, kwa jinsi mifumo yetu ilivyotengenezwa, hakuna njia ya kumuokoa mtu anayebet.

Unadhani natania?

Okay, let me make my case. Makampuni ya kubeti Tanzania ni mangapi?

Nimekuuliza, nijibu.

Hujui?

Okay, ngoja nikusaidie, maana utafanya nini bila mimi?

Kuna makampuni siyo Chini ya 22 ya Kubeti Tanzania, na yote yanataka uweke buku upate kushinda Jackpot ya mabillion ya pesa

Kila kampuni inaonekana ni unique, na “eti” una uwezekano wa kushinda ukibeti na kampuni yao.

Na, ngoja nikuulize swali jingine. Do you know the win rate of these betting games nchini Tanzania? Yaani, unajua ni asilimia ngapi ya watu ambao hubeti kwa siku huishia Kushinda?

Saivi sikusaidii.

Nataka unijibu.

Hata hii hujui mwanangu? aah, basi nshajua itabidi nikusaidie kila kitu sasa.

97% of Betters in Tanzania

Yes, 97% ya wote ambao unasikia wanabeti, hupoteza pesa zao kila wanapobeti. ina maana 3% tu ndo hushinda bets.

Okay, ngoja nikupe perspective.

Survey ya Africa Business Insider kwa Watanzania inaonesha asilimia 71.13% ya vijana wanabeti.

71.13% ya walioulizwa, walisema wanabeti

Kwa mwaka 2018 tu, kulikuwa na vituo zaidi ya 2600 vya kubeti katika miji kama Dar es Salaam. sasa hivi vimeongezeka Mara ngapi?

Kufikia mwaka 2029, tutakuwa na watu wakubeti 224,300 online nchini Tanzania.

Okay, ngoja nikupige na kitu kizito kichwani… On average, watanzania wanaobeti wanabeti 100$ ambayo ni sawa na 250,000/= hivi za kitanzania

Feedinco's 2025 Analysis: An analysis by Feedinco in 2025 estimated that the total annual volume of bets in Tanzania is around $1.2 billion, with an average monthly betting expenditure of about $100 per person.

Kumbuka ni 3% tu hushinda, kwahyo kama Betting volume ya mwaka 2025 ni 1.2$ Billion, watanzania wanapoteza $116.4M sawa na Billion 291 za kitanzania kwenye kubeti

Now, this is Scary.

Inaogopesha sana kama kijana unamaliza chuo na degree yako ambayo mama yako amekusomesha kwa kucheza Vikoba, hujapata Ajira kwasababu hakuna Ajira Mpya, kumbuka umekopeshwa na Heslb unadaiwa sio Chini ya 10M tsh.

Kwahyo unashinda mtandaoni kama vijana wengine wengi kupata Inspiration, na kwa mitandao ilivyotengenezwa, imeundwa kukufanya uvutiwe na Content za Umbea na lifestyle za wasanii

Na bado, hao hao wasanii na watu maarufu unaowatizamia ambao ni marolemodel wako ndo Mstari wa mbele wa kukushawishi uendelee kubeti

Wanalipwa na makampuni ya kubeti kukushawishi uendelee kubaki kwenye kundi la loosers

Kama 97% ya wanaobeti wanapoteza pesa

Ina maana kulibidi kuwepo na jitihada za kuwasaidia wapate ajira, lakini kwa bahati mbaya hakuna,

Kwahyo unabidi utafute namna ya kukwepa kuwa mmoja wa watu kwenye hili kundi

Ni addiction ambayo hakuna mtu mwingine tofauti na mimi anayetaka uondokane nayo

Asilimia kubwa ya Vijana wa kiume waliomaliza vyuo wanabeti tangu wakiwa Vyuoni

Sikulaumu. Sio kosa lako.

Hakuna ajira, na mifumo yote haijatengenezwa kukusaidia Kufanikiwa hata kidogo

Benki hukopesheki kwasababu huna Cashflow,

Kwenye Makampuni huajiriki kwasababu hauna Experience

Huwezi kuanzisha biashara kwasababu huna Mtaji

Serikali haiwezi kukuajiri kwasababu inajaribu kupunguza government expenditure

Wazazi hawawezi kukusaidia kwasababu eti wameshakusomesha, unabidi utafute ajira mwenyewe

Kila mmoja anayekwambia ujiajiri, ameajiriwa. Lakini usimlaumu kwasababu hata yeye Hajui Jinsi ya Kubadilisha Degree yako kuwa Ajira.

Lakini kila mmoja hapo juu, anafaidika na wewe kuendelea kubeti.

Bank haikukopeshi lakini inapata transfer fees

Makampuni hayataki kukuajiri lakini yanawekeza stock na kupata dividends kutoka kwenye share za zabetting companies

Serikali zinapata faida na kodi ushinde au usishinde.

Hakuna anayefaidika ukiacha kubeti, ndo maana wasanii wengi na watu maarufu wanataka uendelee kubeti

Wanalipwa kwa endorsements na partnerships, na wengine wameanzisha makampuni ya kubeti kukubakisha kwenye kundi hili la Losers, asilimia 97%

Japo kuwa pesa ni vizuri kutafuta pesa, lakini sioni kama ni sahihi kutengeneza pesa kwa kumfanya mtu mwingine awe Loser

Hawatutakii mema hawa jamaa

Jikinge na Kubeti

Hii subtitle imenichekesa sana, but anyways…

Now, i have good news for you.

Hivyo ulivyo hapo ulipo, ni sehemu nzuri ya kufanya maamuzi

Ni kama umefika Round about, uko unazunguka tu, hujafanya maamuzi uende exit gani

Hata wewe mwenyewe ndani yako unajua kabisa, ukiendelea kufanya yale ulikuwa ukiyafanya kila siku, yatakupa matokeo yale yale

Ndo maana akili yako imekuwa ikipata mawazo na maswali ya kukupush ufanye maamuzi

Nianzishe biashara?

Nianzishe biashara gani?

Mtaji nitautoa wapi?

Au nikasome masters?

Au nitafute scholarship?

Au nianzishe biashara nichukue mzigo China?

Au nifungue saloon?

Au nianze muziki?

Au nifanye kilimo?

Biashara yangu haipati wateja, nitatoboa kweli?

Au nikope pikipiki, baada ya muda itakuwa ya kwangu?

Maswali yote hayo ni Mungu anakusukuma utoke kwenye Confort Zone. Utoke kwenye Confortability ya kuamini kwamba huenda siku moja kitu kitatokea utashinda bila kufanya big decisions, big changes.

Lakini, maamuzi unaweza kufanya leo. Just Exit.

Yaani, una nyingi za kuchukua kujitoa kwenye Umasikini.

Tatizo haujui ni ipi itakupeleka kule unakotaka kwenda

And that is Good News My friend.

Huenda haujui ukianzisha biashara utapatwa na nini, lakini sote tunajua ukiendelea kukaa hapo ulipo maisha yako yatakuwa vipi

so, let me help you.

Kuna vijana wameusoma Mchezo. Ni asilimia 1% tu ya wahitimu wameweza kufanya hiki kitu nachoenda kukueleza.

Vijana wachache sasa hivi mitandaoni, wakiwemo wahitimu wachache wa Vyuo, wametumia ujuzi na Degree zao kuanzisha Biashara kubwa kuliko hata watu wenye Maduka.

Nakwambia hivi kwasababu kazi yangu kwa hii miaka Miwili, imekuwa ni kuwasaidia hawa watu kuweza kutumia Mitandao ya Kijamii kama Instagram, tiktok pamoja na AI kuweza kuanzisha Biashara kuuza Huduma na Digital Products kwenye social media.

Mimi binafsi, sehemu ya Degree yangu BSc Agricultural Economics & Agribusiness nimefundishwa Service Marketing, ambayo ndiyo biashara ninayofanya sasa hivi.

Hata hivyo, siyo lazima uwe na Degree au uwe genius, ukifuata baadhi ya principles unaweza kutumia vizuri hili wimbi jipya la Uchumi wa Kidigitali ambalo ni 1% tu ya vijama wameweza kulitumia na kufaidika nalo

Na kumbuka, kati ya 10 wanaoanzisha biashara kwenye Mitandao ya Kijamii, 8 wanapata Return on Investment.

Sijui hata kwanini kila mtu hafahamu haya mambo

The 2 Natural Principles

Kwanza kuna Principles mbili kubwa za maisha nilizojifunza miaka hii mitatu ya kufanya biashara yangu.

  1. The Consistency - Compounding Principle

  2. The Principle of Faith

Hizi Principle mbili ndizo huwa zinamsaidia kipofu aweze kutoka kwake asubuhi, na kifimbo chake, na bado akarudi usiku akiwa na furaha kuliko asilimia kubwa ya watu wasio na ulemavu wowote

Hizi principle ndizo zimefanya kila mtu aliyefanikiwa afanikiwe kwa kujua au kutokujua. Wale wanaojua kuzitumia, wamejikuta wakifanikiwa tena na tena na tena.

Wale walioweza kuzitumia hizi principles, wameanzisha biashara na kufanikiwa japokuwa kuna nyakati walipata hasara, walikosa wateja au hata kutengwa na jamii, bado walifanikiwa.

Solutions to Your Problems

Hizi Principles, kama ungependa tuzijadili kwenye barua zijazo nijulishe, kwa leo Ngoja tuangalie Maswali yaliyoko kichwani Mwako na tuyajibu kutumia hizi Principles.

  1. Nianzishe biashara?

    Jibu ni, Je Unataka Kunzisha biashara? Kwasababu, kama unataka kuanzisha Biashara yoyote ile, inawezekana. Swali ni Unataka?

    Ninamfahamu rafiki yangu mmoja alikuwa Monitor wa darasa langu wakati nasoma primary, tulikuwa tukizungumzia biashara tangu tukiwa darasani, na japokuwa kuna vikwazo vingi vya biashara alikutana navyo kuanza, sasa hivi anamiliki moja kati ya Security system companies Mwanza kasababu tu alikuwa Anataka kuanzisha biashara na sio kitu kingine.

    Hakusomea mambo ya security wala kusomea biashara, aliamua kuanza biashara, na sasa hivi niseme “Anaendelea Vizuri”

    Kama unataka kuanzisha biashara, acha kujiuliza maswali mengi. Anzisha biashara.

  2. Nianzishe biashara gani?

    Swali zuri ni, Unataka Kuanzisha Biashara gani? Hili swali nimeongeza ‘unataka’ kwasababu, sheria za Mungu (The Principle of Faith) inasema, Chochote utakachokiomba, amini umeshakipata.

    Kwahyo, ungependa kumiliki biashara gani? Ukishajibu hili swali, anza kulifanyia kazi. Jifunze zaidi kuhusu hyo biashara, soma vitabu, courses, sikiliza podcasts, wasikilize walioianzisha, utajikuta umepata hatua ya kwanza.

    Nilipomaliza Chuo, sikujua nitafanya biashara gani. Lakini nilipojiuliza hili swali, nikaja na wazo la kuwa na kampuni ya Marketing ya Biashara ndogo ndogo za Huduma. Maamuzi yalikuja kwasababu tangu zamani nasaidia wafanyabiashara na Brand Identities na Content creation

    Nikaanza kujifunza, kusoma, kuchukua course etc, na Muda wenyewe uliniletea ZillimDigital a Social Media Marketing platform in Tanzania, sasa hivi tuna Partners zaidi ya 12 kila mwezi ambao tunafanya nao kazi kutangaza biashara kwenye Mitandao ya Kijamii.

    Narudia tena, swali zuri ni “Nataka kuanzisha Biashara gani?”

  3. Mtaji nitautoa wapi?

    Jibu la hili swali nitakalokupatia, linahitaji tu uwe unaniamini. Zaidi ya hapo utahisi nakudanganya.

    Biashara yoyote unayotaka kuanzisha, itatengeneza pesa kama utampa mtu mwingine kitu cha thamani kuliko pesa anayoenda kukulipa.

    Mfano, nikikuuzia kitabu, ukanipa 25,000/- utaondoka ukiamini kwamba, kitabu hicho kina thamani zaidi ya hyo pesa uliyoyotoa.

    Si ndiyo?

    Ngoja sasa nikupe jibu, Huhitaji mtaji kuanzisha Biashara.

    Kabla hujakimbia ukidhani nakupiga kamba, ngoja nikuelezee point yangu, alafu utasema kama nadanganya.

    Tatizo, asilimia kubwa ya watu wanapotaka kuanzisha biashara wanatata waanze kwa kununua mzigo, baadala ya kutafuta watu wanaohitaji mzigo kwanza.

    Siku hizi, kwa kutumia social media marketing, tunafanya Reverse engineering ya hii process, inatusaidia kuanzisha biashara yoyote bila mtaji.

    Changamoto ya hii mbinu ni kwamba, unahitaji kuwa patient na kuamini kwenye The Consistency - Compounding Principle.

  4. Au nikasome masters?

    Swali ni, Unataka kusoma masters? Utaitumia kufanya nini? Unaihitaji? Umeajiriwa unataka kuoneza Ujuzi?

    Hayo ndo maswali yatakayosaidia kufanya maamuzi, mtu yeyote asikwambie haiwezekani. Hata mimi siwezi.

    Nachofahamu, kama unataka kusoma Masters, au Una masters… Unaweza kubadili hyo degree yako kuwa pesa.

    Ukitumia mitandao ya kijamii vizuri, unaweza kubadilisha maisha yako ndani ya Mwezi mmoja.

    Ngoja nikupe story moja.

    Weekend iliyopita, mmoja wa wanafunzi wangu alikuwa anenda kupokea Tuzo ya Kimataifa kutoka Kenya. Japo kuwa huyu mwanafunzi wangu naye amebadili degree yake kuwa Biashara na ndo sababu alikuwa anapokea Tuzo, kwenye Hii story nataka nikuelezee kuhusu mtu niliyekutana naye kwenye hii siku ya Tuzo

    Dada mmoja alikuwa amekaa pembeni yetu kwenye meza, amesoma Bachelor Degree ya Finance kutoka IFM nadhani.

    Alipokea tuzo kwasababu biashara yake ni kuwasaidia wanandoa waweze kupanga bajeti nzuri kila week kwaajiri ya Familia zao

    Hyo ndo Biashara yake.

    Hauzi bidhaa, wala hana duka Kariakoo, lakini biashara yake imetokana na ujuzi wake tu (BSc Finance), tena bila mtaji wowote.

    Mpaka sasa nadhani umeshapata logic ya kutumia kufanya maamuzi na kujibuu maswali yako mengine. Au nianzishe biashara nichukue mzigo China? Au nifungue saloon? Au nianze muziki? Au nifanye kilimo?

Fanya unachotaka kufanya, sasa hivi.

Muda unaoweka kwenye mambo yasiyo na msingi, utakuletea mabadiliko makubwa sana kwenye Maisha yako kama Ukiwekeza kwenye kujijenga mwenyewe na Kujenga Biashara yako.

  1. Hakuna mtu atakayekuja kukuokoa wala kukutoa kwenye trap ambayo mifumo inafaidika nayo.

    Ukitaka kubaki kuwa kwenye kundi la asilimia 97% ya vijana ambao ni wasio na malengo na Maisha yao endelea na siku yako kama kawaida

  2. Lakini kama unataka Kujiunga na 1% ya vijana watanzania ambao hawako perfect, hawajatoka katika mazingira mazuri, hawana support wala utegemezi wa aina yoyote

    Lakini bado kila kukicha wanatumia nguvu, akili na uwezo wao kujiendeleza na hata kutumia mitandao ya kijamii kibiashara… anza leo.

Hawa vijana nawaita The Zillims. Watu wasio na Support yoyote, isipokuwa akili yao tu. Kwa kihaya ukisikia mtu anazungumziwa kwamba ‘Zilimu’ ujue “Japo kuwa hawamuelewi, lakini akili zimo, Nguvu zimo, uwezo umo, Busara zimo” Wanakuunderestimate.

Wewe ni Zillim

Baadala ya kubeti Jackpot, unaweza ukabeti on yourself. Unaweza ukabeti kwamba ukiamua kufanya Biashara au kujijenga, inawezekana.

Ukiamua Kuacha kubeti, Nakupatia kila kitu unachohitaji Kuanzisha na kutangaza Biashara yako kwenye Mitandao ya Kijamii

Zillim. Kijana asiye na Support yoyote, isipokuwa akili yake na Mungu. Kwa kihaya ukisikia mtu anazungumziwa kwamba ‘Zilimu’ ujue “Japo kuwa hawamuelewi, lakini akili zimo, Nguvu zimo, uwezo umo, Busara zimo”

Mimi ni Digital Service Marketing Strategist by Profession, na takwimu zinaonesha Asilimia 83 ya watu wanaoanzisha Biashara kwenye Mitandao ya Kijamii huona faida.

83% mwanangu.

Tukirudi kwenye Kubeti ina maana, mfano kati ya vijana 1000 Tanzania, 713 wanabeti

Kati ya hao ina maana 97% yao wanapoteza pesa kila siku yaani 691 ni Losers

Na, ina maana watu 22 tu ndo wanashinda beti (Kati ya 1000)

The Good News

Lakini, kati ya vijana wale wachache waliobaki, ile asilimia 3% wale wakaanzisha Biashara kwenye Mitandao ya Kijamii, au kuitumia mitandao ya kijamii, Kuwa Mainfluencers, Content Creators, Consultants, Coaches, etc

25 kati ya 30 wanapata faida.

Hii inamaanisha, If you bet on yourself, You win.

Na ukiwin, familia yako Inawin, ndugu zako wanawin, Marafiki zako wanawin. Unakuwa kati ya 1%, na hata mimi Coach wako nitawin

Unapata Influencer Deals, Unakuza network na vyote hivi vinawezekana kama Ukiamua kufanya mabadiliko ndani tu ya miezi mitatu ya Focus.

Mitandao ni nyumbani sasa. We cant escape it. Mimi binafsi Haiwezekani lisaa likapita bila kushika simu yangu

Hivyo, unfollow watu wote ambao hawakusaidii chochote kwenye mitandao, jichimbie kwa siku 30, ujifunze na urudi ukiwa na Vision mpya ya Kuanzisha na Kutangaza Biashara yako

Karibu sana zillim.com

Ninakutakia mafanikio siku zote

Naitwa Elius Kamuhangire

Founder Zillim Digital Marketing Partners

Kama una Biashara au Unataka kuanzisha Biashara kwenye Mitandao ya Kijamii na Umependa hii barua ya leo, Jiunge kwenye Newsletter bora na ya kwanza Dar es Salaam yenye wasomaji zaidi ya 439+, Pia nitakutumia Training ya 1Hr unayoweza kujifunza jinsi ya kutumia mitandao ya Kijamii kujenga Biashara yako

Reply

or to participate.