• Elius' Letters
  • Posts
  • 278: Step-by-Step: Kugeuza Content Isiyouza Kuanza Kuleta Mauzo Haraka

278: Step-by-Step: Kugeuza Content Isiyouza Kuanza Kuleta Mauzo Haraka

Mjasi, nakuandikia hii barua leo kwasababu nimeona Wajasiriamali wengi wanakaa na kujiuliza kwanini content zao hazibadiliki kuwa mauzo, leads, au hata DM zenye maana. Na mara nyingi, tatizo sio kwamba bidhaa yako haivutii, lakini kwa Experience yangu ya kufanya kazi na wataalamu nimegundua ni content zako tu zenyewe hazifanyi kazi yake. Na ntakuonesha mambo 5 ambayo huwa tunafanya.

Barua ya 278. Sababu 5 Kwanini Content Yako Haiconvert

Nilipokuwa nafanya kazi na kijana mmoja Mjasi kutoka Arusha, alikuwa na kila kitu tunachodhani ni formula ya kupata wateja wengi online, Instagram yenye muonekano mzuri na smart, captions zilizopangwa vizuri etc. Lakini baada ya miezi sita, zero sales… mauzo sifur.

Nilimuuliza, “Darasani nimekufundisha Kufanya Analysis, Umeangalia watu wanafanya nini baada ya kusoma post zako?” Akasema, “Wengi wanalike, lakini hakuna anayeuliza bei au kubonyeza link.” Nikamwambia — likes hazilipi kodi, Engagement na DMs ndo zinaleta mauzo.

Mjasi, nakuandikia hii barua leo kwasababu nimeona Wajasiriamali wengi wanakaa na kujiuliza kwanini content zao hazibadiliki kuwa mauzo, leads, au hata DM zenye maana. Na mara nyingi, tatizo sio kwamba bidhaa yako haivutii, lakini kwa Experience yangu ya kufanya kazi na wataalamu nimegundua ni content zako tu zenyewe hazifanyi kazi yake. Na leo ntakuonesha mambo 5 ambayo huwa tunafanya.

Sasa, ni mambo gani yanafanya content zako zisilete mauzo? Twende sasa

1. CTA Isiyoeleweka

Watu wengi wanafikiria kuwa wateja watasoma content, wataelewa product, kisha kwa akili zao tu watakimbilia kukununua. Lakini uhalisia hauko hiyo boss wangu, watu wanahitaji kuambiwa hatua ya kuchukua, kwa maneno clear kabisa na rahisi.

Waambie “Bonyeza link kuagiza sasa,” “Tuma DM neno ‘OFA’ kupata maelezo,” au “Jisajili leo kwa nafasi ya bure.” Nasisitiza jaman, Bila hatua hiyo, mtu ana scroll tu na kuendelea na maisha yake.

2. Audience Isiyo Sahihi

Kama lengo lako ni kupata followers wengi ili kila mtu awe mteja wako, utajikuta unaongea pekee yako mtandaoni. Naandika hii barua asubuhi wakati nimetoka gym, kwaho ngoja nitumie mfano wa Gym. Mfano una biashara ya gym, ukipost kuhusu gym membership lakini followers wako wengi wako kwenye makundi ya wapenda vyakula na muziki, utapata likes kwa sababu ya picha nzuri, lakini hakuna atakayetokea kesho kwenye gym yako. Kwahyo lazima ujue unazungumza na nani, shida zao ni zipi, na lugha gani inawagusa.

3. Quality ya Content Duni

Okay, sasa tuongelee mambo muhimu…. Content yenye makosa makosa, picha zenye blur au picha mbaya mbaya, au video zenye sauti hafifu vinatoa picha kwamba hata product yako inaweza kuwa ya kiwango hicho hicho.

Kuna kitabu kimoja kinaitwa Presuasion by Robert Cialdini anasema Trust aka Uaminifu hujengwa kabla mtu hajatoa hela yake. Hii ndio maana mtu anaweza kuona tu video moja nzuri na akaamua, “Ngoja ninunue kwa Huyu jamaa najua kabisa atanipa kitu kizuri.”

Kwahyo jitahidi utengeneze Content kwa Malengo. Kama huna simu nzuri Omba simu kwa rafiki utengeneze Content nyingi kwa siku moja na uhamishie kwenye simu yako maisha yaendelee au tumia AI kutengeneza Content (Kwenye Madarasa yangu ninafundisha Mbinu za Kutumia AI kupata mauzo na kutengeneza Content)

4. Headlines/ Vichwa vya Habari Dhaifu

Headline ndio kama mhudumu wa mgahawa wako wa content, ikiboa, hakuna atakayeingia na kununua chapati zako. Nimekuwekea screenshot ya Instagram yangu uone jinsi ninavyozitumia kwenye Content zanngu.

Mfano Kuna mteja wangu Alijiunga na madarasa yangu ya Online na anauza skincare na mwanzo alikuwa anaandika headlines kama “Hii ni Bidhaa Bora za Ngozi,” lakini hiyo ni general sana na haitokuleta wateja wa maana.

Lakini alipopita kwenye darasa langu la Content Creator Masterclass akaanza kuandika Headlines kama “Jinsi ya Kupunguza Makovu ya Uso Kwa Wiki 2” akapata wateja zaidi ya 14 siku ya kwanza kwasababu kwenye hiyo headline umeweka curiosity na sababu ya mtu kusoma zaidi au kununu bidhaa/huduma.

5. Hakuna Value Proposition

Value proposition ni ile sentensi au point au hata ishara inayoeleza mtu moja kwa moja, “Hii ndio sababu ya wewe kunichagua.” Inaonesha thamani utakayompa mtu, ndo maana kitaalamu tunaiita Value Proposition au Unique Value Proposition (UVP/USP)

Wakati unajaribu kuonesha thamani yako Usifanye iwe vague kwa kusema “Tunatoa Huduma bora kwa bei nafuu.” Watu wanataka kujua haswa unawaokoa muda? Unawasaidia kuonekana vizuri? Unawapatia faida zaidi ya pesa waliyolipa?

Ngoja nitumie mfano wangu kukueleza kuhusu hii Concept. Mfano, huwa napata wanafunzi wachache sana wanaojiunga kwenye Madarasa yangu ya personal Branding, nadhani kwasababu ada ni kubwa 499k tsh ukilinganisha na wataalamu wengine mtandaoni, lakini ndani ya Miezi mitatu tu baada ya kujiunga na kufanyia kazi mafunzo, wateja wangu wote hujenga Brand zenye Authority Kubwa kuliko hata washindani kwenye Soko lao

Caren Shuubi @pregnancy_nutritiontz Brand #1 ya Lishe kwa Wajawazito na wazazo East Africa Followers 96K ndani ya miezi 8

Lishe na Loy Followers 144k Brand #1 ya Lishe kwa Watoto East Africa

Mr Code TZ ni Suit/Fashion Consultant #1 East Africa Followers 83K ndani ya Miezi Sita

Dr Aurelia Healthy Living ni Daktari #1 wa Afya ya Mfumo wa Umengenyaji Tanzania followers 17K ndani ya miezi 3

Na wengine wengi, Kwahyo kwakifupi (UVP) nawasaidia Kujenga Brand zinazodumu na zenye Authority Mtandaoni zinazowaletea Wateja Zenyewe bila kutumia hata mia kwenye Matangazo. Hyo ndo nguvu ya Value proposition. Ndo inanisaidia kupata wateja wakubwa wanaolipa Vizuri bila kuchelewa.

Aya, tumejadili nini leo?

Conversions au Mauzo Yanakuja Kwa Mkakati (Strategy)

Tulifuata Hatua Hizi… Content Zikaleta Mauzo Haraka

  1. Hakikisha Kila content iwe na CTA safi na ya moja kwa moja.

  2. Ongea na audience sahihi tu, sio kila mtu.

  3. Hakikisha quality ya picha, video, na maandishi yako iko vizuri (Unaweza kutumia AI).

  4. Tumia headlines zenye nguvu na zinazoleta curiosity.

  5. Toa value proposition inayoeleweka na kushawishi bila kuonekana kama unalazimisha mauzo.

Huu mchezo wa content siyo wa kupata likes, ni kuhakikisha kila mtu anayevutiwa anajua hatua ya kuchukua na anaipitia kwa urahisi. Ukitengeneza strategy kwenye vitu hivi, utaona tofauti kubwa kwenye mauzo na leads zako.

Jifunze Kujitangaza Online na AI (na Zillim)

Kama umejifunza kitu leo, usiishie kusoma tu. Fanya mazoezi.

Na kama wewe ni Mjasi au Content Creator uko tayari kujifunza zaidi kuhusu kutumia AI kukuza biashara yako ya mitandaoni na Kujenga Brand inayoshawishi bila kutumia gharama kubwa au kustress kuhusu matangazo na wateja jiunge kwenye Personal Branding Masterclass yetu. Ukijiunga utaweza kupata AI For Social Media Marketing Training pamoja na Social Media Strategy Masterclass BURE.

Nitakupatia pia Mfumo wangu mzima wa AI ninaotumia kuuza na Kupata wateja Online BUREEE.

Uwe na Siku Njema Mjasi, Mimi ni Shabiki yako namba Moja, tutaonana Darasani.

PS: Kama ada ya madarasa yangu ni kikwazo cha Kufanya kazi na mimi au kujiunga, tafadhali naomba usichukulie kama mwisho, lengo langu ni kusaidia Wafanyabiashara walioko Serious Pamoja na wajasi wengi Tanzania Kadri ya Uwezo wangu, hivyo nimetengeneza Chellenge ambayo ndani ya siku 3 tutajifunza pamoja jinsi ya Kutumia AI Kupata wateja na kujenga Brand Mtandaoni kwa tsh 49,500/- tu kujiunga.

Nafasi ziko 20 tu, utapata templates na kila kitu unachohitaji kuanza na nina uhakika Utajifunza vitu vitakavyokusaidia kwa zaidi ya Miaka 10 inayokuja. Nitumie Message Whatsapp Kujiunga.

Reply

or to participate.