- Elius' Marketing Newsletter
- Posts
- Kwanini Hofu ya Kufeli Inauwa Ndoto Yako ya Biashara (na jinsi ya Kujiokoa)
Kwanini Hofu ya Kufeli Inauwa Ndoto Yako ya Biashara (na jinsi ya Kujiokoa)
Una miaka 24-35 na biashara yako haina muelekeo mzuri, hupati wateja na hauna Consistency kwenye Kuwapata na kutengeneza Content, itakuwa Hujapitia Training Ya Kuanzisha Na Kutangaza Biashara yako kwenye Mitandao ya Kijamii ambayo ni Free kwa Subscribers wa hii Newsletter, Tafadhali Click hapa kujiunga BURE
Mara ngapi umepata wazo kali la biashara, ukaanza kulifanyia research, ukaandika kila kitu chini, ukapanga kila hatua… lakini hujaanza?
Umejiambia labda bado hujajipanga vizuri, labda kuna vitu zaidi vya kujifunza, au labda unasubiri wakati sahihi.
Ukweli ni mmoja—woga wa kufeli unakuzuia kuchukua hatua, na kama hautaujua na kuudhibiti, utaangamiza ndoto yako kabla hata haijaanza.
Leo kwenye hii barua, tunajadili jinsi woga wa kufeli unavyokwamisha maendeleo yako na hatua unazoweza kuchukua ili kuuondoa kabisa.
1. Woga Unakufanya Ujikute Unawaza Kupita Kiasi (Paralysis by Analysis)
Kuna watu wanapenda kufikiria sana kabla ya kuchukua hatua hasa zinazohitaji uvumilivu na investment ya muda na pesa.
Wanaangalia video nyingi, wanapitia kozi mbalimbali, wanaandika business plans za kurasa 20, lakini mwisho wa siku hawachukui hatua yoyote.
Hii tunaiita paralysis by analysis—unafikiria sana kiasi kwamba unashindwa kuchukua hatua.
But honestly, mawazo pekee hayawezi kukufikisha popote.
Hakuna biashara inayokua kwa sababu mmiliki wake alikaa mwaka mzima akifikiria tu. Au kuna mmoja unamfahamu unipe mfano?
Hakuna mafanikio yanayopatikana kwa sababu tu ulichanganua kila kitu kabla ya kuanza.
So, katika kusoma kwangu vitabu na kuchelewa chelewa kuanza mambo, nimejifunza kama unataka kujiondoa kwenye hii hali, tumia kanuni ya 24-HOUR RULE.
Ukipata wazo la biashara leo, chukua hatua moja ndogo ndani ya masaa 24.
Hata kama ni kufungua akaunti ya Instagram kwa hiyo biashara, kutafuta jina, au kuulizia bidhaa sokoni, fanya kitu.
Hatua ndogo inakupa momentum ya kusonga mbele.
2. Woga wa Maneno ya Watu (Watu Watasema)
Hii ni moja ya sababu kuu zinazowazuia wengi kuanzisha biashara.
"Nikiweka biashara yangu online, watu wataniona vipi?"
"Wakisema biashara yangu ni ndogo sana?"
"Wakicheka?"
Kama kuna kitu unatakiwa kuelewa, ni hiki: watu wanasema kila siku, haijalishi unafanya nini.
Hata ukiamua kutokufanya chochote, bado kuna mtu atakusema.
Ukianza biashara na ikashindwa, watu watasema.
Ukianzisha na ikafanikiwa, watu bado watasema.
Kwa hiyo, kwa nini ujizuie kwa sababu ya watu?
Ni bora uanze na upambane, kuliko ukae kimya huku ukiwaza jinsi watu wanavyokuchukulia.
Watu hawawezi kukulisha, hawawezi kulipa bills zako, kodi, bando, na hawawezi kuishi maisha yako kwa niaba yako.
Wewe ndiye mwenye wajibu wa kuendesha ndoto yako, sio wao.
Ikiwa woga huu unakushika sana, basi jifunze kuzoea kutokusikiliza maoni yasiyokujenga.
Focus kwenye watu wanaokusaidia kukua, sio wanaokurudisha nyuma.
3. Woga wa Kupoteza Pesa
Kila mtu anaogopa kupoteza pesa.
Ni kawaida.
Lakini woga huu unakuangamiza kwa sababu unakuweka kwenye hali ya kutokuwa in motion.
Unakaa ukihofia kuwa ukianzisha biashara utapata hasara, lakini huangalii upande mwingine—je, ukifanikiwa?
Biashara yoyote ina risk.
Lakini pia, kukaa bila kufanya kitu nacho ni risk.
Muda unavyoenda, nafasi nzuri zinapotea, na mtu mwingine anachukua nafasi yako.
Mfanyabiashara yeyote aliyefanikiwa, hata wale wakubwa unaowajua, amewahi kupoteza pesa.
Jeff Bezos alipoteza mamilioni ya dola kabla Amazon haijafanikiwa.
Elon Musk alifilisika mara kadhaa kabla SpaceX na Tesla hazijawa kampuni kubwa.
Kama unaogopa kupoteza pesa, basi chukua hatua kwa njia ambayo ina risk ndogo.
Usianze na mtaji mkubwa—anza na mtaji mdogo kwanza.
Test market, ona mwitikio wa wateja, na rekebisha biashara yako taratibu.
Kupoteza kidogo na kujifunza ni bora kuliko kukaa bila kufanya chochote.
4. Woga wa Kuanza Bila Plan
Watu wengi wanajidanganya kwamba wanahitaji kuwa na complete business plan kabla ya kuanza biashara.
Wanaandika business plans za kurasa 50, wanataka kila kitu kiwe tayari, wanasubiri wakati sahihi… na miaka inapita hawajaanza.
Ukweli ni huu—hakuna wakati sahihi wa kuanza.
Hakuna biashara iliyoanza ikiwa tayari kwa asilimia 100.
Mfano mzuri ni kijana mmoja Dar es Salaam ambaye alitaka kufungua duka la Fashion… mteja wangu Emmanuel.
Alikuwa anataka apate stock kamili kabla ya kuanza.
Aliposhauriwa aanze na kidogo alichonacho, alifungua na akaanza na suit alizonazo tangu zamani.
Wateja walivyokuja, wakaanza kuulizia kama anaweza kuwashonea, ndipo akaongeza taratibu.
Leo ana team kubwa ya mafundi na brand yake ya EHB suits inafanya vizuri, na hakusubiri mpaka kila kitu kiwe tayari.
Hii inaitwa lean startup approach—anza na kile ulichonacho, then boresha biashara yako unavyoendelea.
5. Woga wa Kufeli Kwenyewe
Watu wengi wanaogopa kufeli kiasi kwamba wanashindwa kabisa kuchukua hatua yoyote.
Lakini kitu ambacho wanakosa kuelewa ni kwamba woga wa kufeli ndio failure yenyewe.
Mtu ambaye hajawahi kujaribu kitu chochote kwa sababu anaogopa kufeli tayari ameshindwa.
Kwanini? Kwa sababu tayari hajachukua hatua.
Watu wote waliowahi kufanikiwa walifeli kwanza kabla ya kupata mafanikio.
Steve Jobs alifukuzwa Apple kabla ya kurudi na kulifanya kuwa kampuni kubwa.
Oprah alifukuzwa kwenye kazi ya kwanza kwa sababu waliamini hana kipaji cha kutangaza kwenye TV.
Jack Ma alikataliwa kazi ya KFC.
Kila mmoja wao alifeli, lakini walijifunza kutoka kwenye makosa yao.
Kama unataka kufanikiwa, unahitaji kuanza kuona failure kama sehemu ya safari.
Unapofeli, unajifunza kitu kipya ambacho kinakusogeza karibu na mafanikio.
Unapojifunza kutokana na makosa, unapata nafasi ya kufanya vizuri zaidi next time.
Challenge ya Week Hii
Sasa nataka nikupatie Challenge.
Chukua dakika moja, tafakari ni kitu gani umekuwa ukiogopa kuanza kwa sababu ya woga wa kufeli.
Kisha jiulize: ni hatua gani moja ndogo naweza kuchukua leo ili kusogea karibu na ndoto yangu?
Hatua hiyo inaweza kuwa kuandika wazo lako chini, kufungua akaunti ya biashara kwenye mitandao ya kijamii, kutafuta supplier, au hata kuzungumza na mtu anayefanya kile unachotaka kufanya.
Chochote utakachofanya, hakikisha unachukua hatua leo.
Usiruhusu woga uangamize ndoto yako.
Anza sasa, jifunze njiani, na usikubali hofu ikuondoe kwenye njia yako ya mafanikio.
Kama una maoni au unataka kushiriki Challenge yako, jibu email hii au uniachie comment.
Na kama unataka newsletter kama hii kila wiki, hakikisha umesubscribe.
Tuonane wiki ijayo kwa somo lingine lenye nguvu.
ps: Una miaka 24-35 na biashara yako haina muelekeo mzuri, hupati wateja na hauna Consistency kwenye Kuwapata na kutengeneza Content, itakuwa Hujapitia Training Ya Kuanzisha Na Kutangaza Biashara yako kwenye Mitandao ya Kijamii ambayo ni Free kwa Subscribers wa hii Newsletter, Tafadhali Click hapa kujiunga BURE
Reply