- Elius' Marketing Newsletter
- Posts
- Jinsi Washindani Wakubwa Wanavyosaidiana (Ndiyo, Inatokea!)
Jinsi Washindani Wakubwa Wanavyosaidiana (Ndiyo, Inatokea!)
Kila kampuni inajitangaza kwa nguvu, na hii imefanya soko la soda likue worldwide. Kama unanifuatilia Youtube, naifananishaga hii vita kama ya Diamond na Alikiba. Indirectly, hawa jamaa wamesaidiana sana, ndo maana hawataki ugomvi uishe.
Unajua ile vibe ya ushindani mkali? Coca-Cola vs. Pepsi, Apple vs. Microsoft, Ford vs. GM… But what if I told you kwamba kuna moments ambapo hawa ma-giants wamepeana mkono wa msaada badala ya kupigana? (Ntakupa mifano hivi pubde) lakini…
Imagine uko kwenye biashara yako, unahangaika, pesa mtaji umeanza kuisha, halafu mshindani wako mkubwa anakuja anakusaidia kusimama tena.
Sounds crazy, right? But hii imeshatokea mara nyingi kwenye dunia ya biashara.
Apple & Microsoft – Kutoka kuwa Maadui Mpaka Msaada wa Milioni
1997, Apple ilikuwa kwenye hali mbaya, almost kufa kabisa. Fuatilia vizuri story za Steve Jobs utagundua. Nani alikuja kuokoa? Microsoft! Bill Gates alichomoa $150M ku-invest kwenye Apple na wakakubaliana kuendelea kutengeneza Microsoft Office kwenye Mac.
Bila hii move, huenda leo tusingekuwa na iPhones. (Maskini iphone yangu🥹)
2. Coca-Cola & Pepsi – Ushindani Tunaoupenda sasa
Wamepigana kwenye marketing kwa miaka, lakini indirectly wamekua wakisaidiana.
Kila kampuni inajitangaza kwa nguvu, na hii imefanya soko la soda likue worldwide. Kama unanifuatilia Youtube, naifananishaga hii vita kama ya Diamond na Alikiba. Indirectly, hawa jamaa wamesaidiana sana, ndo maana hawataki ugomvi uishe.
Fun fact: Coca na Pepsi, Kuna maeneo fulani duniani wanashare hata bottling facilities kupunguza gharama!
3. Ford & General Motors – Washindani Lakini Wanaendesha Gari Moja
Hawa ni wapinzani wakubwa kwenye magari, lakini guess what? Walishirikiana kutengeneza 10-speed automatic transmission inayotumika kwenye Ford F-150 na Chevy Camaro ZL1.
Kila mmoja alipunguza R&D costs, na wote wakaibuka na teknolojia bora zaidi.
4. Samsung & Apple – Adui Yako Anaweza Kuwa Supplier Wako
Unajua Apple inategemea Samsung kwa OLED displays za iPhones? Yes, Iphone zote zinatumia Screen za Samsung!
Hawa jamaa wanashindana kwenye smartphones lakini behind the scenes Apple inanunua displays kutoka kwa Samsung kwa billions!
Ushindani unakuwa mbele ya pazia, biashara nyuma ya pazia.
5. Amazon & Best Buy – Kuuza Bidhaa za Mshindani Wako
Amazon ni tishio kubwa kwa Supermarket za Electronics zinaitwa Best Buy, lakini badala ya kugombana, Best Buy ilikubali kuuza Fire TV-powered smart TVs kutoka Amazon.
Amazon ikapata market penetration, Best Buy ikapata exclusive models.
Bado unadhani washindani wako ni maadui zako? Unachekesha sana. Ngoja nikupe nyingine…
6. Google & Apple – Biashara Inazidi Ushindani
Kama unatumia vifaa vya apple, Iphones na Mac kama mimi hehehe… utagudua Apple anatumia Google kama default search engine kwenye Safari (Safari ni Default Browser ya Apple).
Guess what? Google huwa analipa Apple billions kila mwaka kwa hii deal!
Badala ya Apple kutengeneza search engine yake, wanafaidika na pesa kutoka kwa mshindani wao mkubwa.
Sababu kubwa ya Kukupa huu ujumbe:
Ushindani ni mzuri, lakini kuna moments ambapo strategic collaboration inalipa zaidi kuliko vita.
Wafanyabiashara wengi wadogo washamba wanachukuliaga ushindani serious kiasi kwamba unageuka chuki na Ushirikina hahaha Usione kila mshindani kama adui, sometimes wanaweza kuwa sababu ya mafanikio yako!
Mimi kazi yangu kubwa ni kukusaidia Kujenga Biashara inayodumu miaka mingi, kwa kukupa mfumo mzuri wa kujenga Personal Brand yako wewe na wafanyabiashara wengine kama mimi na wewe! (Text DM)
You Are Your Biggest Competitor – Wewe Ndio Mshindani Wako Mwenyewe
Si mshindani wako wa nje, si mtu mwingine—ni wewe!Unajizuia mwenyewe kwa:
❌ Kutojifunza – Unataka matokeo mapya lakini unashikilia mindset ya zamani.
❌ Kutojitangaza vizuri – Watu wanapaswa kukutafuta badala ya wewe kujitokeza? Hapana!
❌ Kufocus tu kwenye kuuza – Biashara ni mahusiano, si tu miamala.
❌ Kutowekeza kwenye uhusiano na wateja – Watu hununua kutoka kwa watu wanaowaamini.
❌ Kukosa kujiamini – Kama hujiamini, nani atakuamini?
Huyo ndiye mshindani wako halisi. Na ukimshinda yeye, hakuna atakayeweza kukuzuia! Kama unapambana na kujitangaza sokoni, huenda unahitaji “washindani” wa kukusukuma mbele. Karibu Zillim Growth Partners – Let’s talk!
Elius Kamuhangire
Creator, Zillim Digital
Reply