Mbinu 3 za Jinsi ya Kuvutia Wateja Hata Kama Soko Limejaa Washindani!

Najua kuna wakati unaangalia social media mnaona kila mtu anafanya biashara, kila mtu ni content creator, kila mtu anasema 'this is the best way to make money.' Lakini ukifuata hizi hatua 3, Utakwepa ushindani wowote kwenye Biashara yako.

If you are a young entrepreneur, freelancer, or digital creator trying to stand out in this crowded online world—leo ni siku yako!

Kabla tuzame kwenye barua ya leo, kwa wale wasionifahamu, Naitwa Elius Kauhangire, ni mtaalamu wa Marketing and sales, na mwanzilishi wa Zillim Marketing Partners ambayo ni njia yangu ya kuwasaidia vijana wafanyabiashara kukuza ujuzi wa biashara na kuongeza mauzo kutumia mitandao ya kijamii.

Nakutangazia kwamba nimeandaa darasa jingine la masaa mawili BURE kwa wasomaji wangu.

Hili darasa litakuonesha mbinu zote kwa kina ambazo nimetumia kuwasaidia wafanyabiashara wengine waweze kuongeza mauzo kwenye biashara zao. Darasa hili limeandaliwa kwa zaidi ya miezi minne, na waliolipitia wamelipa 350,000 kulitizama, mimi nakupatia wewe Bure.

Hili hapa chini, wahi kabla kila mtu hajaiangalia, Nimekuonesha na Mifumo kabisa, kwahyo utacopy na kupaste kwenye biashara yako.

Nitaliondoa baada ya muda mfupi:

Tuendelee…

Najua kuna wakati unaangalia social media mnaona kila mtu anafanya biashara, kila mtu ni content creator, kila mtu anasema 'this is the best way to make money.'

Na unaanza kujiuliza, nafanyaje kujitofautisha? Kama kila mtu anafanya hii kitu, why should people pick me?

Haya ndo maswali aliyoniuliza mteja mwanafunzi wangu weekend iliopita kwenye kikao.

Leo tutaongelea How to Stand Out in a Saturated Market When You're Just Starting Out.

Hii kitu ya kusema soko limejaa ni uongo. Hii ni psychological barrier ambayo inakufanya uogope kuanza au kuwa mbunifu kutumia mitandao. Let me tell you something—

  • Kuna watu wengi wanauza nguo, lakini bado kuna brands mpya zinaibuka na zinauza sana. Mfano Kariakoo, kuna maduka mengi ya Nguo na bado nina marafiki wengi pale wana maduka na wanaweka maduka mapya ya nguo

  • Kuna watu wengi wanafundisha digital marketing, but people still look for new perspectives.

  • Kuna watu wengi wanafanya content creation, but not everyone connects with the same audience.

SasaThe 3 Strategies to Stand Out

1. Be Authentically You

Watu hawapendi biashara yako—wanapenda wewe! Your personality, your story, your journey ndiyo inafanya watu wakuamini.

Ukianza biashara ya freelancing kwa mfano, usijaribu kuwa kama wale ma-expert wa miaka 10. Watu wanataka kuona safari yako kama beginner—wanataka mtu wanayeweza ku-relate naye.

Ukianza biashara ya beauty products, watu hawapendi tu product, wanataka story ya kwa nini unaipenda, umeitumia vipi, na kwa nini wao waitumie.

Nimekuelezea mbinu tunayotumia kujitofautisha kwenye video hapo juu.

Jiposition kwa kuwa original. Hakuna competition kwa kitu ambacho ni cha kipekee kutoka kwako.

2. Solve a Specific Problem for a Specific Person

Kama unajaribu kuuza kila kitu kwa kila mtu, utashindwa. You need to niche down!

Nimefanya biashara mtandaoni tangu 2019, lakini nimekuwa mwanafunzi wa Digital marketing tangu 2023 October nilipokuwa nimeajiriwa na nikapata ajali ya Gari.

Nikajiuliza, kama sitaki tena kufanya kazi za kuamka azubuhi kwenda kazini, nahitaji nifanye nini?

Nikaingia industry ya Digital Marketing na kujifunza, kutafuta macoach, kusoma Courses etc… sasa kwa kawaida ungetegemea kwamba ningeenda kuomba ajira sehemu, lakini sikufanya hivyo.

Niliamua kutumia ujuzi wangu kuanza kuwasaidia Vijana wa Tanzania wenye Biashara waweze kutangaza na kukuza biashara zao na kutengeneza Pesa kutumia mitandao ya kijamii, kitu ambacho kwangu ni rahisi kufanya.

Hii ndiyo tofauti kati ya mtu anayema, 'Nafanya marketing,' na mtu anasema, 'Nawasaidia SMEs Tanzania kupata wateja kupitia organic social media.' - mimi.

See the difference?

  • Kama unafanya content ya tech, be specific: “Ninafundisha watu jinsi ya kutumia AI kuongeza productivity kazini” instead of “Naongelea teknolojia”

  • Kama unauza skincare, be specific: “Nasaidia wanawake wa Tanzania wenye oily skin kupata glow natural” instead of “Nauza skincare”

  • Kama unauza nguo, be specific: “Nasaidia wanaume kustyle Jeans na mashati kwaajiri ya Official Look'“ baadala ya kusema “Tunauza majeans”

Be laser-focused. When you speak to everyone, you speak to no one.

3. Be Consistently Visible, Onekana kila mara.

Unaweza kuwa na idea nzuri lakini kama huna visibility, huonekani, nobody will notice. Na hapa ndipo watu wengi wanafeli.

Sasa jiulize, 'Am I showing up enough?'

  • Kama uko Instagram, are you posting reels daily?

  • Kama uko YouTube, are you putting out long-form content weekly?

  • Kama uko TikTok, are you leveraging trends + originality? maana hizo ndo sifa kubwa za Tiktok algorith

Consistency beats talent. You don’t need to be the best—you just need to show up more than the rest.

Alright nimekufundisha zaidi kwenye video hapo juu, lakini pia, leo nataka uweke hii knowledge kwa action, ukaifanyie kazi:

  1. Andika nini kinakufanya unique/uwe tofauti – Je, ni personality yako? Story yako? Ujuzi wako?

  2. Define niche yako – Unahudumia nani? Unamsaidiaje?

  3. Commit to being visible – Set a goal ya how often utapost na uifuate! Unataka upost Mara Moja kwa siku? au mara sita kwa week, au mara mbili kwa siku?

Tizama hiyo video ni darasa la Masaa mawili mwanzo mpaka mwisho, itabadilisha jinsi unavyofanya Biashara mtandaoni, na mwisho. nitakuonesha mbinu ninayotumia kuongeza mauzo kwenye Biashara zangu na biashara za wateja wangu!

Kumbuka: The market is NOT too crowded.

Ni wale ambao wanajitofautisha ndio wanashinda. Sasa ni wakati wako kusimama na kuonekana!

Your Friend in Business

Elius Kamuhangire McBenvivs

ps: Kama wewe ni mgeni hapa, tafadhali subscribe kwenye hizi barua, nitakuwa nakutumia mwenyewe kwenye Inbox yako. Subscribe hapo chini

Reply

or to participate.