The 3-Step Formula KuClose More Sales Online

Kwa bahati nzuri, mimi ni mtafiti mambo, na utafiti wangu ulinipelekea kwenye mpangilio wa hatua za kuwavutia watu kama unataka wawezekane kununua.

Mjasi niaje?

2024 ilikuwa mwaka wa kujifunza mengi, nilikaa siku moja nikishangaa kwa nini biashara yangu online haikui kama deni la taifa. Nilikuwa napost kila siku, lakini wateja walikuwa hawananunui.

Nikaanza kujiuliza, “Hivi kuna siri gani hapa ambayo sijui?” Kama wewe unapambana na hili, najua unanielewa—kuna tofauti kubwa kati ya kuonyesha bidhaa na kufunga mauzo.

Kwa bahati nzuri, mimi ni mtu wa kutafiti mambo, na utafiti wangu ulinipelekea kwenye hizi mpangilio wa hatua za kuwavutia watu kama unataka wawezekane kununua.

Leo nakuletea formula rahisi ya hatua 3 ambayo itakusaidia kuuza zaidi bila kuhisi kama unawalazimisha wateja.

1. Vuta Attention – Usibaki Kwenye Kivuli

Kama hakuna anayekuona, hakuna atakayenunua. Nilijifunza hili kwa njia ngumu sana—kuweka tu bidhaa au kupost kuhusu huduma yako online hatoshi.

Unahitaji content zinayovutia macho ya wateja wako, na nimegundua pia kwamba mara nyingi sio lazima kutumia mbinu za ajabu. Ni maneno tu unayozungumza.

Badala ya kusema “Tunauza viatu vya quality,” sema “Umechoka viatu vinavyopasuka ndani ya miezi mitatu? Hii hapa suluhisho.” Boom! mnaweza kuwa mnauza kitu kile kile, lakini nikuhakikishie huyu wa pili hatopata hasara kama ya TTCL.

Lakini pia ni muhimu kujua unavutia nani—Mac na Cathy wote wanataka bidhaa nzuri, lakini njia ya kuwapata ni tofauti. Unapofahamu shida ya mteja wako, content zako zitawavuta wenye shida hiyo moja kwa moja.

2. Toa Sababu ya Kukuamini – Hakuna Anayenunua Kama Hana Uhakika

Watu wananunua kutoka kwa wale wanaowaamini. Hapo ndipo nilipogundua nguvu ya social proof. Weka reviews za wateja waliopata matokeo au share ushuhuda wao.

Kama unauza Course kama mimi au unafanya Consultation, toa offer ya bure ili waone thamani ya kazi yako. Kama ni bidhaa, onesha before na after. Mjasi, nakuhakikishia mtu yeyote anayetaka unachouza atanunua akiona wengine wameshafanikiwa kwa kufanya kazi na wewe.

Hakikisha unaonyesha hilo ili wawe na uhakika wa kukuchagua.

3. Call to Action – Mwambie Mteja Afanye Nini

Mara nyingi nilipoteza mauzo kwa sababu sikuwapa wateja hatua wazi ya kufuata kufanya kazi na mimi.

Wengi hawatanunua kama hawajui cha kufanya baada ya kukuona. Usiseme tu “Wasiliana nasi”—hiyo ni vague sana. Sema “Bonyeza link kwenye bio kuagiza sasa” au “Nitext DM leo.”

Ongeza “haraka” kama unachouza ni limited offer au bonus kwa wanaochukua ASAP. Usifanye watu wafikirie sana—kama una kitu kizuri, waelekeze moja kwa moja jinsi ya kukipata.

Hii Ndiyo Safari Yako

Kufunga mauzo zaidi online sio ngumu ukifata hizi hatua 3: Vuta attention ya watu, wape sababu ya kukuamini, na uwaelekeze wafanye nini.

Nilipoanza kutumia hii formula, nikaona tofauti kubwa kwenye biashara yangu.

Lakini sasa kumbuka, growth kwenye project yoyote haiji overnight—ni kama kupanda mti, unahitaji kuendelea kuumwagilia. Usikate tamaa mwanangu, matokeo yanakuja.

Na kama unataka Mfumo wa mauzo unaofanya kazi 24/7

Mimi na team yangu tuko hapa kwa ajili yako. Kwa muda wa wiki chache tu, tunauza Social Media Business Playbook yetu kwa 47,000/- pekee. Hii ni guide ya hatua kwa hatua kujenga na kutangaza biashara online kwa mtu anayeanza kujifunza—jinsi ya kupata wateja na kufunga mauzo bila stress.

Jipatie ya kwako ili usiwe wakubahatisha Biashara online, Nitumie DM neno “PLAYBOOK” kupata ya kwako sasa hivi.

Elius Kamuhangire
Mjasi/Zillim

Mjasi/Zillim is any entrepreneur who embraces digital growth, leverages content marketing, and continuously adapts to build a thriving, future-proof business.

Reply

or to participate.