- Elius' Letters
- Posts
- Mteja Mmoja Anavyoweza Kuamua Hatma ya Biashara Yako Nzima
Mteja Mmoja Anavyoweza Kuamua Hatma ya Biashara Yako Nzima
Gundua namna mawazo na vitendo vidogo—kama post moja Instagram au glasi ya maji asubuhi—vinaweza kubadilisha afya, biashara, na uhusiano wako mzima.
Goodmorning Mjasi,
Today should be. agreat day.
Yesterday nililala mapema, kwahyo nimefanikiwa kuamshwa na alarm yangu ya saa kumi na moja. Siku nyingine huwa inapiga kelele lakini siamki, leo nimeamka.
Kuna video niliangalia jana usiku kabla sijalala, na nimegundua ina maana sana kwahyo nataka nishare na wewe.
Kwenye hii video, Michael Talbot ambaye ni mwandishi wa vitabu mmarekani, kwenye miaka ya 80, alikuwa anahojiwa kwenye TV na kusuggest kwamba ulimwengu wetu ni Hologram kama TV. Kila tunachokiona ni kama tunaangalia picha kwenye TV na ubongo wetu ndo hyo tv inayovuta hyo picha na kukuonesha
Kwa kifupi, alikuwa anasema:
Ulimwengu unaweza kuwa kama Hologram. Kila sehemu ndogo ya ulimwengu (grain of sand, tone moja ya mwanga, au chembe ndogo ya mwili wetu) inabeba picha nzima ya ulimwengu.
Akili zetu pia zinafanya kazi kwa mfumo huo huo wa hologram, kumbukumbu na uzoefu wetu zikiwa zimegawanyika lakini kila sehemu ndogo bado ina picha nzima.
Hii inamaanisha kitu kikubwa sana: hatutenganishwi. Wewe na mimi ni kitu komoja, mwili na akili, biashara na maisha binafsi vyote vimeunganishwa kama sehemu za picha moja.
Pia alieleza kwamba kile tunachoamini kwenye akili zetu kinaweza kuunda matokeo ya kweli. Mfano ni wagonjwa mahospitalini ambao huwa wanapona kwa dawa feki (zinaitwa placebo kwa lugha ya kidaktari), kwa sababu waliamini kweli kwamba dawa itawaponya.
Kwa hivyo, nguvu ya akili yetu na imani zetu inaweza kubadilisha miili yetu, biashara zetu, na hata mahusiano yetu.
Na pia, ndo maana kwenye hili Darasa la masaa matatu ambalo limeonwa na watu 65 mpaka sasa, nimefundisha jinsi ya kutumia AI kupata wateja mtandaoni kwasababu internet nzima inaendeshwa na AI.
Mfano Rahisi: Biashara na Afya
Fikiria unamiliki duka Kariakoo kwa mfano.
Siku moja unajitahidi kumhudumia mteja mmoja vizuri sana unamsikiliza, unampa ushauri, na unamshukuru.
Wengine wanaweza kuona kama ni jambo dogo, “ni mteja mmoja tu.”
Lakini kumbe, huyu mteja mmoja anaakisi picha kubwa ya biashara yako yote. Atawaambia rafiki zake, ataandika review, na ataamua kama arudi tena.
Kwa lugha ya hologram, mteja mmoja = soko lote limebeba picha yake.
Au kwenye afya:
Kunywa glasi moja ya maji kila asubuhi ni hatua ndogo.
Lakini hatua hiyo ndogo inaakisi afya yako yote mwili wako unapata nguvu, akili yako inafanya kazi vizuri, hata mood yako inabadilika.
Hii ndiyo Michael Talbot alikuwa anamaanisha kwenye Video: kila sehemu ndogo ya maisha yako inabeba picha kubwa ya maisha yako yote.
Kwa lugha rahisi: maisha yako ni hologram. Kila wazo dogo, kila hatua ndogo, kila uhusiano mdogo unaakisi picha kubwa ya maisha yako yote.
Sasa Mjasi, ukiona kwamba kila sehemu ya maisha yako inabeba picha nzima, utaishi kwa makini zaidi. Post moja Instagram inaweza kuonyesha brand yako nzima. Mazoezi madogo kila siku yanaweza kubadilisha afya yako. Tabasamu moja linaweza kuokoa uhusiano mzima.
Na, leo unaweza kubadilisha biashara yako yote na jinsi unavyotumia instagram kwa kujifunza jinsi ya kutumia AI kujenga brand yako Mtandaoni, hata kama una Followers wachache.
Kwenye hii video pia ukiangalia nzima, nimeeleza vizuri jinsi ya Kujiunga na private group langu la wanafunzi wangu utajifunza jinsi ya kutengeneza pesa Online kwa kufanya kazi masaa manne tu kwa week.
Uwe na Siku njema Mjasi
Elius Kamuhangire McBenvics
Creator | Zillim
Reply