Jinsi ya Kudeal na Business Rejection Bila Kukata Tamaa

Leo, nimejifunza kitu kimoja—kukataliwa kwako na wateja au Clients au hata business Partners hakumaanishi biashara yako haina thamani. Inamaanisha tu kuwa huyo mtu hakuwa sahihi kwako. Kama wewe ni Mjasi na umekuwa unakataliwa mara kwa mara, hii ndio njia ya kuendelea bila kukata tamaa.

Nakumbuka siku moja nilim-DM client ambaye niliona anaweza kufaidika na huduma zangu. Nilikuwa nimeandika message safi, nikaijenga vizuri kabisa kama Shaaban Robert. Nikaibonyeza send

Baada ya dakika tano, jamaa akajibu:
"asante dogo."

Bro, hiyo kitu iliuma! Nilikaa nikijiuliza, Hivi kweli biashara yangu ina maana? Labda huduma yangu haijakamilika? Labda mimi ndo shida? alafu… hili lijamaa linaniita dogo? Mimi Mhaya kabisa? huyu mjinga hajui kwamba nimeishi Marekani?

Okay, hapo nimeweka Sodium Chloride nyingi… Sikusema hayo yote lakini kiukweli iliniuma sana.

Lakini leo, nimejifunza kitu kimoja—kukataliwa kwako na wateja au Clients au hata business Partners hakumaanishi biashara yako haina thamani. Inamaanisha tu kuwa huyo mtu hakuwa sahihi kwako. Kama wewe ni Mjasi na umekuwa unakataliwa mara kwa mara, hii ndio njia ya kuendelea bila kukata tamaa.

1. Usichukulie Personal

Wajasi wengi wanachukulia rejection kama "proof" kwamba biashara yao haifai. But listen, rejection haikuhusu wewe, ni inamhusu zaidi yule mtu anayekataa.

  • Wengine hawako tayari kwa kile unachotoa, and thats okay

  • Wengine hawana bajeti bado, and thats okay

  • Wengine wanaogopa kujaribu kitu kipya, and thats okay

Kwahyo, usiruhusu mtu mmoja akufanye uhisi kama huwezi kufanikiwa.

2. Kumbuka: Kila “Hapana” Ni Hatua Moja Karibu na “Ndiyo”

Hapa ndo mindset ya Wajasi waliofanikiwa inatofautiana na wale wanaoishia njiani.

Nilipomaliza Chuo, nilifanya kazi kwenye Branch moja ya Bank kubwa sana Tanzania (Benki ya Blue - ushaifahamu nadhani), na nilikuwa nasaidia kuuza Bima za Magari.

Sasa kama umewahi utakuwa unajua ile system ya kuuza bima, Wanaambiwa hivi:
"For every 10 rejections, one person will say yes."

Sasa imagine ungekuwa unajua kabisa kwamba baada ya kukataliwa mara 10, client mmoja atakubali. Je, ungekata tamaa baada ya kukataliwa na mteja wa kwanza?

Rejection sio mwisho, ni sehemu ya process. Wajasi wanaojua hili wanakazana mpaka wanapata "ndiyo."

(Btw, kama uko Single pia, hii strategy bado inafanya kazi unaweza kuitumia… niliijaribu na Shemeji yako anakusalimia niko nae hapa)

Okay, tuendelee na huu walaka wa Mtume Kamuhangire kwa Wajasi…

3. Tafuta Lessons Kwenye Rejection

Rejection inaweza kuwa feedback bora kama ukiichukulia positively.

Badala ya kusema: "Mimi siwezi," jiulize:

  • Kwa nini huyu client hakunihitaji?

  • Niliwasilisha vipi huduma yangu?

  • Kuna kitu naweza kuboresha?

Nilijifunza hili somo wakati nafanya kazi kwenye Mgahawa (Ndiyo, wakati naishi Marekani… Yes, sasa utafanyaje, ndo ishatokea sasa)… Anyway Siku moja, walikuja wanafunzi kama saba wakaagiza msosi mwingi, wakala kidogo alafu wkaondoka.

Sasa, kijana wako mimi Customer service, wakatu wanakuja kulipia, sikujali kuuliza kwanini wamekataa chakula. Nikawalipisha, nikawaambia “Gudnight” haha

Boss wangu Michael, ambaye ndo namwita Coach wangu wa kwanza wa Customer Relationship Management, akaona akaniuliza “Umewauliza kwanini wameacha Chakula?”

Nikasema “Wamelipa”

Akakimbia nje kuwasimamisha, akawarudisha ndani. Akaniita “tu”kawauliza shida nini “Mbona mmeacha chakula”

Kumbe, Kwakuwa ilikuwa Restaurant ya vyakula vya Ki-asia, waliagiza vitu ambavyo walikuwa hawavielewi (Si unajua mambo ya Nyoka na Konokono)

Kwahyo, tukajifunza kwamba Tunahitaji kubalilisha Description ya Menu, na matangazo kwenye Website

Kuhusu nyoka natania, lakini my Point is Sometimes, watu wanakataa sio kwa sababu huduma yako ni mbaya, bali kwa sababu hujajua kuiuza vizuri.

4. Wajasi Waliofanikiwa Walikataliwa Zaidi Kuliko Wewe

Ukiona unakataliwa, kumbuka tu kwamba hata watu wakubwa walipitia hapo.

  • Jack Ma (Aliyeanzisha Alibaba ambayo mnanunua bidhaa za China) alikataliwa kufanya kazi KFC

  • J.K. Rowling alikataliwa na wachapishaji zaidi ya mara 12 kabla Harry Potter haijakubaliwa

  • Harmonize aliambiwa asante kwa Kushiriki kabla hajaanza kuimba Kiingereza

Kama hawa wote waliweza kusimama baada ya kukataliwa, wewe unalia nini sasa?

5. Endelea Kujaribu Bila Hofu

Wajasi wengi wanaogopa rejection kiasi kwamba wanaacha kujaribu kabisa. Lakini hapa ndio ukweli mchungu: Ukiogopa kukataliwa, umeamua kuwa Kashuma milele.

The only way to win is to keep pushing. Hakuna njia nyingine.

  • Ukikataliwa na Mteja mmoja, Mtafute mteja mwingine

  • Ukikosa matokeo kwa Post moja, Post tena

  • Simu, Piga simu nyingine

  • Fanya follow-up

The more you try, the more you increase your chances of getting a YES.

Kashuma ni mtu yeyote anayetamani maendeleo, lakini anapinga mabadiliko, anaendelea kushikilia mbinu za kizamani za biashara, na anakwepa kujifunza, jambo linalomfanya ashindwe kushindana katika dunia ya kisasa ya kidigitali.

6. Reframe Rejection: "Si Sasa, Labda Baadaye"

Mteja akisema hapana leo haimaanishi atasema hapana milele.

  • Labda hana bajeti sasa hivi

  • Labda hajaona thamani sasa hivi

  • Labda bado hajawa na urgency ya tatizo lake, hana haraka.

Nimepata clients wengi sana walionikataa mwaka mmoja uliopita, lakini walirudi baada ya muda walipokuwa tayari. Kwa hiyo, usichukue rejection kama mwisho, chukulia kama "sio sasa hivi, labda baadaye”.

7. Punguza Muda wa Kukasirika, Ongeza Muda wa Kutafuta Fursa Mpya

Ukikataliwa, usikae siku nzima ukihisi vibaya. Weka limit ya dakika 10 za kukasirika, halafu move on.

Kama unataka support ya jinsi ya kujenga mifumo itakayokupatia wateja na kukua kwenye biashara yako bila kuogopa rejection, DM me. Let’s grow together.

Elius Kamuhangire
Zillim Strategist

Mjasi/Zillim ni anyone who embraces digital growth, leverages content marketing, and continuously adapts to build a thriving, future-proof business.

A Kashuma ni mtu yeyote anayepinga mabadiliko, anayeendelea kushikilia mbinu za kizamani za biashara, na anayekwepa kujifunza, jambo linalomfanya ashindwe kushindana katika dunia ya kisasa ya kidigitali.

Reply

or to participate.