Jinsi ya Kucheza na Malengo yako

Hivi ndivyo mimi hufanya kuudanganya Ubongo ili nitimize Malengo yangu, hatua kwa hatua

Habari za asubuhi Partners. 

Leo nimeamka nikapitia Somo la siku ya sita (kwa wale walioko kwenye Program yetu ya 30 Days Social Media Creator) ambalo kama umekwishalipitia unajua tulizungumzia jinsi ya kuweka malengo yako mapya kwaajiri ya Biashara yako.

Naomba kusisitiza kwamba, katika jitihada zako za kutengeneza pesa kwenye mitando ya kijamii au biashara yako, Malengo yako ni muhimu kuliko hata mauzo. 

Ofcourse, naelewa ukipata mauzo mengi utafurahi sana, lakini Ubongo wa Binadamu haujaumbwa kuridhika baada ya kupata matokeo.

Ubongo wetu umeumbwa kufurahi pale unapokuona ukipiga hatua kuyafikia Malengo yako.

Ndo maana hata utajirike kiasi gani, huwezi kusema “sasa nimeshatajirika, kuanzia leo sifanyi kazi, ni kula na kulala”

Mara nyingi watu hukata tamaa katika biashara zao sio kwasababu hawatengenezi pesa, bali kwasababu hawana Motivation ya kuendelea kupambana na kuvumilia pale ambapo hawaoni matokeo.

Swali ni, Je, wale ambao hawakati tamaa, motivation wanaitoa wapi? Wale ambao hawapati mauzo mengi mwanzoni, na sometimes wanapata hasara mwanzoni tena kwa muda mrefu kabla hawajaanza kuiona faida, ni kitu gani huwa kinawakeep moving?

Swali zuri.

Kabla sijakupa jibu rahisi, naomba nikuelezee Chemistry ya ubongo wa binadamu kwa urahisi

Tutumie Mfano: Ukiambiwa ulime shamba mpaka liishe (bila kuambiwa ni Hekari ngapi wala kuoneshwa linaishia wapi), utawahi kuchoka na utateseka kufanya hyo kazi. Si ndiyo?

Lakini ukiambiwa ni Hekari 20 na unaweza kulima masaa kadhaa kwa siku, (japokuwa ni nyingi, au ndogo kulinganisha na Kabila unalotoka) utafanya kwa nguvu umalize, kwasababu kila unapomaliza Hekari moja unajiona ukisogea mbele.

Sasa ubongo, ubongo unakuwa unafanya hivi.

1. Unapomaliza heka ya kwanza, ubongo unazalisha kemikali inaitwa Dopamine, kukupongeza. (Seriously)

2. ⁠Hyo kemikali ni moja ya kemikali za Furaha, na inakufanya ujisikie vizuri sana.

3. ⁠Inakupa motivation ya kuanza kulima Heka nyingine ili ujisikie furaha tena na uendelee ili utimize lengo lako la kumaliza Heka zote 20.

4. ⁠Ukimaliza heka 10, ubongo unazidi kucelebrate kwasababu umemaliza nusu ya kazi, na umesogea!

Sasa naomba unielewe kitu kimoja hapa, japokuwa yule wa kwanza (ambaye hakujua ni Heka ngapi analima) naye anaweza kuwa analima hekari 20… hatokuwa na motivation kwasababu UBONGO wake hauna vipimo vinavyoashiria kwamba anasogea ili uzalishe kemikali ya Dopamine na kumpa motivation!

Sijui unanipata?

Sasa, turudi kwenye biashara yako!

Unapojiwekea malengo yanayofikika (mfano useme unataka upate followers 1000 mwezi huu kwenye account yako ya Instagram)

Ubongo wako unaanza kufanya ubunifu kukusaidia kufikia lengo lako, na hata pale unapoanza kusogea mfano ukafikia followers 200, japokuwa ni wachache bado, ubongo wako utafurahi kwamba unaelekea kufikia lengo lako.

Na utakapofikia lengo (followers 1000), ubongo unakuzawadia Dopamine kukupa Motivation ili uzidi kupambania malengo yako zaidi.

Njia nyingine muhimu ya kuufanya Ubongo ukupe motivation kila wakati, ni Kusherekea Hatua ndogo ndogo unazopiga!

1. Umepata mteja mmoja? Jipongeze

2. Umepata likes 10 instagram? Jipongeze

3. ⁠Umeweza kutengeneza video yako ya kwanza? Jipongeze

4. ⁠Umemaliza kusoma kitabu? Jipongeze

5. ⁠Umejifunza kitu kipya kuhusu jinsi ya kutangaza Biashara yako? Jipongeze

6. ⁠Umefanya mauzo zaidi ya mwezi ulopita? Jipongeze

7. ⁠Umejifunza kitu kipya kuhusu wateja wako? Jipongeze

Ukufanya hivyo, unakuwa una’hack (au niseme kuuseduce) ubongo wako kupata motivation!

Na sio kwamba unajidanganya, kubuka Lile swali uliloniuliza: Je, wale ambao hawakati tamaa, motivation wanaitoa wapi? Wale ambao hawapati mauzo mengi mwanzoni, na sometimes wanapata hasara mwanzoni tena kwa muda mrefu kabla hawajaanza kuiona faida, ni kitu gani huwa kinawakeep moving?

Jibu ninkwamba, wanaelewa nguvu ya Compounding actions kwamba kuweka jitihada kidogo kidogo zinazokusaidia kupiga hatua ndogo ndogo ndani ya muda mfupi, zitakuletea matokeo makubwa sana ndani ya Muda mrefu!

Hivyo, wanatumia hii mbinu kucelebrate kila hatua ndogo wanayopiga!

Vitu ni vingi vya kucelebrate kwenye Biashara yako! Na ukifanya hivi kila siku, utashangaa jinsi ambavyo utazidi kuona mafanikio kwenye Biashara yako!

Usifocus kwenye mambo negative yanayotokea kwenye Biashara yako! Yataufanya ubongo wako ushindwe kukupa dopamine! Utapata uoga! Fear ni moja ya inhibitors za Dopamine! Utakosa motivation!

Focus kwenye vihatua vidogovidogo unavyopiga kulingana na malengo ulojiwekea!

Sifa kuu ya hayo malengo kama tulivyojifunza kwenye Somo la 6

- Yawe mahsusi, yanapimika, yanahusiana na biashara yako na yanafikika ndani ya Muda maalumu! (This is very Important)

‼️ Yasiwe marahisi kiasi kwamba hayakupi challenge wakati wa kuyafikia, na yasiwe magumu kiasi kwamba yanakatisha tamaa!

Nimekuandikieni hii Barua kukusisitizia jinsi somo letu hili ni Muhimu!

Na nakutakia mafanikio kwenye Biashara yako!

Uwe na siku njema leo!

Iko mikononi mwako!

Kamuhangire (@mcbenvics)

Reply

or to participate.