- Elius' Marketing Newsletter
- Posts
- Kwanini Baadhi Wanatengeneza Pesa Online & Wengine Hapana
Kwanini Baadhi Wanatengeneza Pesa Online & Wengine Hapana
Kila siku tunawaona watu online—wengine wanatoboa, wengine wanahangaika kwa miaka bila kuona matokeo. Sasa swali linakuja, kwa nini wengine wanafanikiwa na wengine wanabaki wakihustle bila breakthrough?
Why Some People Make Money Online & Others Don’t
Mambo vipi Mjasi!
Kila siku tunawaona watu online—wengine wanatoboa, wengine wanahangaika kwa miaka bila kuona matokeo. Sasa swali linakuja, kwa nini wengine wanafanikiwa na wengine wanabaki wakihustle bila breakthrough?
Leo, tunavunja hii topic down kwa uhalisia. And by the end of this, utajua exactly what separates the winners from the strugglers online.
You see, wakati naanza hii kazi, sikujua kwamba kuna tofauti kubwa ya kimawazo kati ya vijana wengi niliotegemea kufanya nao kazi. Wazungu wanaiita Mindset.
Mara nyingi unakuta kitu kinachokufanya ustruggle ungeweza kukitatua kwa kubadilisha jinsi tu unavyofikiria kuhusu hilo jambo.
Kabla sijadive kukupa madini, ngoja nikupe Story. Kuna binti mmoja amesoma Sheria, na ana Masters kabisa. Ana degree nzuri sana tena ana akili nyingi tu kwa mtanzamo wangu.
Siku moja alibook appointment na mimi, alikuwa anataka ushauri kuhusu jinsi ya kutangaza Biashara yake ya nguo na anajiuliza afanyeje ili biashara yake ipate wateja… akaja hapa ofsini tukakaa chini kujadili.
Nikamshauri, baadala ya kuuza nguo… kwanini usibadili hyo degree ulonayo kuwa biashara? Naweza kukusaidia.
Nikamwambia “unaweza kufanya biashara ukiuza ujuzi wa Sheria ya biashara au kitu kama hicho, ukawasaidia wafanyabiashara, au unaweza kufanya sheria ya ndoa ukawasaidia wanandoa kwenye mambo ya kisheria, na ukawapata wateja wengi mtandaoni”
Akanisikiliza wee, lakini akawa HAAMINI kwamba inawezekana. Akawa haamini kwamba ana uwezo wa kujenga biashara kubwa namna hyo.
Akang’ang’ania kufanya biashara ya nguo.
Sasa, kwa mtazamo wangu, nilikuwa naona kwamba, nguvu zote anazojaribu kuweka kwenye business ya nguo, tungefocus kwenye biashara ya Sheria, ndani ya Miaka mitano tungetengeneza Faida kubwa kuliko watu wengine wakubwa wanaouza nguo maana competition ni kubwa (japo kuwa zipo mbinu nyingi za jinsi ya kukwepa competition… ntakufundisha kwenye barua zijazo)
Basi, akawa amekataa anataka auze nguo za kike. Imagine, alinilipa 447,000/- ya consultation, na bado akakataa ushauri wangu.
Cha ajabu, hyo hyo siku ya consultation. Alikuwa anakuja jamaa mwingine kwaajiri ya Consultation, na guess what? Amesoma sheria na yeye alikuwa anataka aanze biashara ya kuuza hardware
Nikampa ushauri huo huo.
Fortunately, akakubali kuanza biashara ya Sheria, tena akachagua kufanya biashara ya Kusaidia watu kusajili makampuni na kufanya compliance. Hii ilikuwa ni mwezi wa saba mwaka 2024, sasa hivi napoandika barua hii, huyu jamaa anapata wateja wengi sana mtandaoni mpaka wengine anawakataa
Tena, mauzo yake kwa siku ni makubwa sana kuliko wauza nguo wote naowafahamu. Jana amepiga simu anasema ameuza huduma ya 3M, kwa siku.
Now, the point of this story, sio kusema kwamba bidhaa haziuzi na unahitaji degree kufanya biashara, hapana. Japokuwa nimewasaidia vijana wengi kubadili degree zao kuwa biashara, thats not my point.
Point yangu ni kwamba, unahitaji New Information kuhusu biashara yako au new ideas ili mindset yako iweze kubadilika, uweze kuona fursa pale ulipo na uweze kuzitumia na kupitia hizi barua zangu, i hope utakuwa unapata taarifa mpya ambazo najitahidi kukutumia
So, lets talk about kwanini baadhi ya watu online unaowafahamu wanatengeneza pesa, na wengine wanashindwa
1. Wanajua Rules za Game
Making money online siyo bahati. Wale wanaofanikiwa wanajua rules of the game—Sheria za mchezo wanajua algorithms, content strategy, audience psychology, na most importantly, jinsi ya kuuza bila kuonekana kama wanauza.
Wale ambao hawatoboi? Wanaingia game bila kuelewa nani wanam-target, nini wanauza, na kwa style gani. Wanatumia muda mwingi kuiga wengine badala ya kujifunza mfumo unaofanya kazi kwao.
Seriously: Kama hujui unacheza game gani, hutashinda!
Simple Rules of the Game
•Ili kuwa mshindi katika mchezo lazima uucheze.
•Ili uushinde mchezo lazima uelewe mchezo unavyochezwa
•Ili uucheze vizuri, wasikilize Makocha zako au wanaoucheza
•Lazima ujue kwamba, Unacheza Mchezo
•Lazima ucheze mchezo ulio ndani ya uwezo wako… x.com/i/web/status/1…— McBenvics (@mcbenvics)
8:07 AM • Feb 4, 2025
2. Wana Clarity ya What They Offer
Huwezi kupata pesa online kama watu hawajui unawasaidiaje wateja wako. Hii ndiyo sababu influencers, digital marketers, na consultants wanaopata hela kubwa wanajulikana kwa kitu kimoja fulani.
Kama ni fitness coach, be the go-to person kwa watu wanaotaka six-pack.
Kama ni marketing expert, be the plug kwa wanaotaka kujua ads zinavyofanya kazi.
Kama ni UGC creator, jenga brand inayovutia brands kufanya kazi na wewe.
Kama ni mwanamziki, basi uwe na style unique kiasi kwamba huwezi kufananishwa na wengine
Kama unauza nguo, jenga utofauti ieleweke unauza nguo aina gani kwa watu gani
Wale wasiopata pesa, Hawakai kwenye niche moja, wanajaribu kila kitu, wanabounce from idea to idea.
Leo unauza hiki
Kesho unauza kile kingine kwasababu umesikia kinalipa
Kila wakati unapobadilisha, unaanza moja.
Think about it like this: Umepanda mbegu ambayo inachukua muda kidogo kuchipua. Alafu, kwakuwa hujui science ya Seed Germination, baada ya week mbili unaamua kutifua na kuanza upya, kisa eti zile mbegu hazijazaa.
Hivyo ndivyo wengi wanafanya kwa kubadilisha biashara kila kukicha.
3. Wana Consistency Beyond Feelings
Success ya online inahitaji consistency ya kijinga sana—yaani, unabidi upost hata kama uko down, fanya kazi hata kama hauna motisha, endelea hata kama unaona no results.
Wengi wanaanza na energy kubwa, wakiona views hazipandi, wanakata tamaa. Lakini wale wanaofanikiwa wanaendelea mpaka wanajulikana.
Moja kati ya wanafunzi wangu ni mwanamuziki. Na japo kuwa ana mambo mengi ya kujifunza bado, anajitahidi sana kuwa Consistent kwenye kupost content.
Tumeanza kufanya kazi pamoja miezi michache iliopita, na sasa hivi naona views kwenye account yake zinaongezeka.
Sio kwamba ameanza kuwafikia watu wapya wengi, la Hasha (Sijawahi kutumia La Hasha kwenye Uandishi wangu, leo kwa mara ya kwanza)… views zimeongezeka kwasababu consistency imemsaidia amweze kupost mara nyingi ndani ya muda mfupi kama tulivyokuwa tumekubaliana
Kwahyo sasa Usiache hadi watu waanze kukuuliza, “Bro, unafanyaje?” Hapo ndo utajua umefika.
4. Wanajua Kuuza Bila Kuomba Omba
Siri moja ya watu wanaotengeneza hela online ni hii: wanaelewa psychology ya selling. Hawapost tu random content halafu wanategemea watu wanunue.
Wanajenga trust.
Wanatoa value kabla ya kuuza.
Wanatengeneza urgency & FOMO kwa audience yao.
Unajua, juzi nilikutana na mwanafunzi wangu mmoja pale Mlimani city… (Yeah, wanafunzi wangu huwa sometimes tunakutana out kama vile hatuko kazini kabisa). Akawa anasema, “Changamoto yangu kubwa ni kwamba sipati wateja wakati kila siku natangaza bidhaa zangu Instagram”
Tukafungua Instagram. Nikamwambia “Changamoto yako kubwa ni kwamba hupati wateja kwasababu kila siku unatangaza bidhaa zako Instagram”
Funny right? Kama umeangalia hii video utagundua kwamba, ukiwa na biashara mtandaoni, wateja wako ni binadamu tu kama wewe na watanunua kutoka kwa mtu wanayemuamini, na wanamuamini mtu wanayemheshimu.
Na unfanyaje kujenga Heshima kwwa wateja wako? Strategy.
Wale wasiopata hela Wanapost vitu vizuri lakini hawaelewi strategy ya kuziconvert into sales.
5. Wanainvest kwa Kujifunza & Tools Sahihi
Huwezi kudaka hela kubwa kama hutaki kuweka hela kwenye knowledge na tools zinazorahisisha kazi. Watu wanaofanikiwa wana invest kwenye courses, mentorship, na vifaa vya kazi.
Siku moja nilienda supermarket, pale mcity. Wakati nazunguka nikakutana na jamaa anauza saa kali mule ndani. Na, week nzima nilikuwa nshajisemea “Nahitaji saa. Tena saa Kali kabisa. Tena sio moja, nataka saa kama tatu”
Sasa hizi saa zinauza laki mbili- tatu hivi nadhani, nikaamua nizchane na saa. At the same time, nikaingia kwenye bookstore nikaondoka na vitabu kama sita vya biashara na Self help, vya laki saba na nusu.
Wale wasiopata hela? Wanataka kila kitu kiwe free. Wanadhani YouTube tutorials zinatosha, hawataki kulipia mentorship, wanangoja miujiza.
Ukweli ni huu: Kama hutaki ku-invest kwenye skills zako, usitegemee watu wakulipe. Hutaki kujifunza Content marketing, hutaki kujifunza jinsi ya kushawishi, hutaki kujifunza chochote, lakini unataka Return on Investment Kubwa? Kwa Investment gani sasa ndugu mteja Kipenzi?
Ukweli ni huu: Kama hutaki ku-invest kwenye skills zako, usitegemee watu wakulipe.
Hutaki kujifunza Content marketing, hutaki kujifunza jinsi ya kushawishi, hutaki kujifunza chochote, lakini unataka Return on Investment Kubwa? Kwa Investment gani sasa ndugu? x.com/i/web/status/1…— McBenvics (@mcbenvics)
6:42 AM • Feb 4, 2025
6. Wanajua Branding na Storytelling
People don’t buy what you sell, they buy who you are. Wale wanaofanikiwa online wanajua jinsi ya ku-connect emotionally na audience yao.
Wale wasiopata hela? Wanapost tu content za kuuza, hakuna emotion, hakuna human touch, hakuna reason ya mtu kujali.
Niligundua hiki kitu miaka mitatu baada ya kuanza kutumia mitandao kibiashara. Nilidhani watu wananunua tu kwasababu wanahitaji bidhaa. I was Wrong.
Watu wanavutiwa na uhalisia wako kuliko hata bidhaa yako. Kwahyo unahitaji kuwa storyteller mzuri.
Na, usidhani kwamba storytelling ni jambo gumu hata kidogo. Mbona tukikutana utaanza kunielezea jinsi Dar kulivyo na joto, na jinsi ambavyo weekend iliopita ulikuwa samaki samaki.
Thats a great stoory, sasa mbona inapokuja kwenye kuongea na wateja unakosa maneno? Brand yako inatengenezwa na Story zako, hivyo ndivyo utakavyojitofautisha kwasababu hakuna mtu mwenye story na Experiences kama zako.
Upo Kwenye Upande Gani?
Ukijiangalia kwa hii list, unajiona wapi?
Kama unajiona kwenye team ya wanaofail, don’t panic. Ni suala la kurekebisha strategy na kuwa intentional, yaani kufanya kwa maksudi
Kama upo kwenye team ya wanaofanikiwa, ongeza efforts!
Hii ni game ya kujituma, consistency, na kujifunza kila siku. Success online haiji kwa bahati—inaletwa na mfumo unaofanya kazi!
Let’s Talk!
Je, wewe unapitia changamoto gani kwenye hii safari ya kutengeneza hela online? Ni kitu gani kinakushikilia nyuma?
Reply to this email na share thoughts zako. Au better yet, tuonane kwenye podcast episode hii weekend ambapo nitachambua hii topic LIVE!
Tuko pamoja,
Elius Kamuhangire
P.S. – Unataka Kuongeza Kipato Online Bila Kuhangaika?
Jiunge na Zillim Digital Academy, ambapo tunakufundisha step-by-step jinsi ya kutengeneza hela online bila kupoteza muda. Unajua what to do —click hapa kupata maelezo ya kujiunga!
Reply