- Elius' Marketing Newsletter
- Posts
- Unaogopa Kupost? Hii Itakusaidia!
Unaogopa Kupost? Hii Itakusaidia!
Kama wewe ni Mjasi na unahisi hofu ya kupost, najua exactly unachopitia. Lakini leo, nataka nikuoneshe njia za kupambana na hii hofu na kuanza kupost kwa confidence.
Skia Mjasi,
Nakumbuka siku yangu ya kwanza kupost video yangu ya kwanza nikiwa na lengo kwenye social media. Nilikuwa na wasiwasi, mikono inatetemeka, moyo unadunda. Nilijiambia, "Watu watasema nini? Nitachekwa?"
Nilikaa na video kwenye draft kwa siku tatu. Kila nikitaka kupost, sauti moja kichwani ilikuwa inanizuia: "Labda haijakamilika… Kuna kitu sijaongea vizuri… Labda nitaposti nikitengeneza nyingine nzuri zaidi… aah kulalek"
Kama wewe ni Mjasi na unahisi hofu ya kupost, najua exactly unachopitia. Lakini leo, nataka nikuoneshe njia za kupambana na hii hofu na kuanza kupost kwa confidence. Leo. Okay, Tuanze ya kwanza…
1. Tambua Hofu Yako Inatoka Wapi
Wajasi wengi wanahofia kupost kwa sababu wanajali sana wanachofikiria watu. But let’s be real—watu hawakufuatilii kama unavyodhani.
Wengi wako busy na maisha yao, kwenye daladala huko wameshikilia kile chuma cha kushika
Wale wanaokudharau hawajawahi hata kujaribu kufanya unachofanya, wanashinda tu kwenye page za umbea wanamsema Zuchu
Na kama kuna atakayekusema vibaya, trust me, huyo hakuwa mteja wako hata kidogo.
Ukishajua kuwa hofu yako haina msingi halisi, unapata nguvu ya kuendelea.
2. Accept That Your First Posts Won’t Be Perfect
Siri moja kubwa ya content creation ni hii: Ukiangalia post zako za mwaka jana na usijione umekuwa bora, basi hujakua. Ngoja nikupe habari mbaya… Post zako za kwanza zitakuwa mbovu sana.
Hii inamaanisha kwamba, unapaswa kuruhusu version yako ya leo iwe mbaya ili version yako ya kesho iwe bora. Hakuna shortcut.
The only way to get good at posting is to actually start posting. Mimi kila siku najifunza kakitu. The more I do it the better I get. Kwahyo, japokuwa napost content zinazoweza kumsaidia mtu mwingine, sana sana zinanisaidia mimi kujifunza na kuwa Creative.
Jifanyie.
3. Start Small, Build Up
Usijilazimishe kuanza na video ya dakika 10 na ukawa super confident. Anza na kitu kidogo:
Post quote yenye caption fupi
Piga selfie na uandike ujumbe mfupi kutoka kwenye mawazo yako
Post video ya sekunde 10 ukiwaambia watu jina lako na unachofanya na uwaambie wakufollow.
Kadri unavyopost kidogo kidogo, confidence inakua naturally. Lengo lanngu lilikuwa kupost video ndefu 50 youtube zinazofundisha kitu. Ya kwanza ilikuwa mbaya, na sijawahi hata kurudia kuiangalia
Sasa hivi nimepost video zaidi ya 100, na naona niko more confident sasa hivi kuongea kwenye Camera kuliko nilipoanza.
Anza kidogo.
4. Jifunze Kujipenda Kwa Sauti Yako & Muonekano Wako
Wajasi wengi wanachukia kusikia sauti zao kwenye video.Team yangu walikuwa wanashangaa nikiwatumia video zangu wareview, nawakataza kuisikiliza mbele yangu… nilikuwa sipendi kusikia sauti yangu. Lakini kadri ninavyoendelea nagundua Ukweli ni kwamba, sauti nnayoisikia kwenye recording ni sauti ambayo watu wamekuwa wakisikia maisha yao yote.
Kama wao wameizoea, kwanini mimi njione tofauti?
Jifunze kuaccept your voice. Accept your look. Ukishajikubali, hakuna mtu atakayeweza kuku-discourage.
Jikubali.
5. Think About Who You’re Helping
Ukiogopa kupost, focus kwa mtu ambaye post yako itamfaa. Kuna Mjasi mwingine au mteja wako huko nje ambaye anasubiri inspiration kutoka kwako au kuelewa umuhimu wa huduma au bidhaa zako. Kuna mtu anayehitaji kusikia kile unachojua au ujumbe ambao Jehova Shama ameweka ndani yako.
Ukijua kwamba content yako inaweza kumsaidia mtu, unakuwa na sababu ya kupost hata kama unaogopa.
(ooh, Ndiyo, hapa namzungumzia Jehova Shama yule anayeimbwaga na Rose Muhando)
Anyways.. tuendelee
6. Weka Target Ya Video 10 Bila Kujali Matokeo
Challenge yako iwe hivi: Post video 10 bila kuangalia likes, comments, au views. Mteja wangu mmoja ni Pharmacist, alipomaliza Chuo akapelekwa kufanya Internship kijijini huko ndani ndani, akawa anashindwa kufanya Content kujenga brand yake… eti.
Assignment yangu ya kwanza kwake ilikuwa hii; Tengeneza Video 10 bila kujali matokeo.
Lengo ni kupata momentum, sio matokeo. Kufika video ya 10, utagundua kuwa hofu yako imepungua.
7. Hakuna Aliyeanza Akawa Mkamilifu – Start Anyway!
Kila content creator mkubwa ulimwenguni alianza na video za kawaida. Hakuna aliyeanza akiwa perfect. Hormozi mwenyewe alianzia kwenye kabati lake la nguo, mimi nafanyia gereji.
The difference between wale waliotoboa na wale walioachia njiani ni moja tu: Waliamua kupost hata walipoogopa.
Leo, nataka ufanye kitu kimoja: Chukua simu yako, tengeneza video fupi, na ipost. Usifikirie sana, just do it!
Ukitaka support zaidi kwenye journey yako ya kuwa confident online na Kujenga Brand inayovutia Opportunities, DM me. Let’s grow together.
Elius Kamuhangire
Zillim
A Zillim/Mjasi is anyone who embraces digital growth, leverages content marketing, and continuously adapts to build a thriving, future-proof business.
Reply