- Elius' Letters
- Posts
- Kwanini Siku Hizi Huna Wateja Wengi Bila Kujitangaza kwa Kulipia Matangazo?
Kwanini Siku Hizi Huna Wateja Wengi Bila Kujitangaza kwa Kulipia Matangazo?
Miezi michache ilopita nilianzisha Program ya Marketers "Lunch and Learn" Kukutana na Online Entrepreneurs, Coaches, Consultants na Wateja wangu for Lunch, kujifunza pamoja na kushare Ideas kuhusu Kupata wateja (Customer Acquisition), Kila mmoja malalamiko yalikuwa, yanahusu kupata wateja bila kutumia ADs. Na leo ntakueleza kwanini.
Kwanini Bado Huna Wateja Wengi Bila Kujitangaza kwa Kulipia?
Kama umegundua hizi week Chache Kila siku unapost Unafanya bidii Unajituma kutengeneza Content.
Lakini bado… kimya. Hakuna wateja wa kutosha Unless uweke bajeti kubwa ya Sponsored ads
Inakatisha tamaa, si ndiyo? Enhee
Miezi michache ilopita nilianzisha Program ya Marketers Lunch and Learn Kukutana na Small Business Owners na Wateja wangu for Lunch, kujifunza pamoja na kushare Ideas kuhusu Kupata wateja (Customer Acquisition),
Kila mmoja alikuwa anaonesha wasiwasi kwenye hili Suala, Anauliza “McBenvics, mbona nikiacha Kurusha Matangazo, IG sipati wateja?”
Mjadala ulikuwa wa moto sana lakini kuna ukweli mchungu ambao wengi hawataki kukubali:
Wateja hawaji because hujawapa sababu ya wao kukuamini.
Na hapa siongelei content tu. Na siongelei caption nzuri au kufanya live tiktok mara moja moja.
Naongelea maamuzi madogo unayofanya kila siku—kuandika post bila kujua unamzungumzia nani… kujaribu kuuza kabla hujatoa thamani yoyote… kukaa kimya ukisubiri DM badala ya kuanza mazungumzo na potential Clients etc.
Matangazo ya kulipia yamekuwa Demokrasia sasa hivi na kila mtu anayafanya na yamefanya wateja wapunguze Imani juu ya biashara mpya na wamekuwa very skeptical wasije “wakapigwa”
Unajua kwanini biashara nyingine za Wajasi na watu wengine online wana biashara ambazo zinaonekana zinakua bila hata kutumia ads?
Sio kwa sababu wana followers wengi. Ni kwa sababu wameamua kujitofautisha kwa njia moja:
Wamejenga imani kabla ya kuuza.
Wameamua kuelewa mteja mmoja kabla ya kulenga wengi.
Wameamua kuonyesha kazi yao badala ya kuisema tu.
Wameamua kutoa stori badala ya kuzungumzia bei.
Wameamua kusikiliza kuliko kulazimisha wateja.
Kama unataka mabadiliko kwenye biashara, usianze na mbinu tu.
Anza na uamuzi:
Je, niko tayari kujenga biashara inayoaminika?
Wateja wanataka kuamini kabla ya kununua.
Na hiyo haijengwi kwa pesa. Haijengwi kwa kubahatisha.
Hujengwa kwa msimamo, uthubutu, na uwazi wa nia yako.
Lakini mwisho wa Mjadala tuliondoka na Mbinu nyingi za kupata wateja Online Bila kutumia Sponsored ADs mbazo mpaka sas tumeona hizi Nane zinafanya kazo na kwenye Training ya hii week nimekufundisha Bure Kabisa ndani ya Dakika kumi.
Tutaonana huko.
– Elius Kamuhangire McBenvics
Zillim.com | Instagram @mcbenvics
Reply